16 Alipokuwa anapita kando ya ziwa Galilaya, aliwaona wavuvi wawili: Simoni na Andrea ndugu yake wakivua samaki kwa wavu.

17 Yesu akawaambia, "Nifuateni nami nitawafanya ninyi wavuvi wa watu."

18 Mara wakaziacha nyavu zao, wakamfuata.